Black Ninjah🇹🇿 · May 17, 2026
Mama unakumbuka vyema sana, Mi kwenda shule ilikuwa mtiti/ Ingawa ulinihusia ukanipiga sana stiki/ Nilichopenda zaidi kufanya ilikuwa mziki/ Now here I am, kila kona sa' nna mashabiki/ Siko home nanyi tena, lebo imeni sign/ Imeniahidi kuniwekea mipango kwenye line/ Nakula nalala nawekewa bando niko fine/ Nikiamini kuwa ntapata urahisi wa mambo kidizain/ Nna gari mama, napiga nalo sana picha/ Mitandaoni ndo navimba nalo sana insta/ Bata ndo usiseme viwanja vyote nishafika/ SamakiSamaki Mbudya Kidimbwi na kadharika/ Najua unashangaa, mambo nayokusimulia/ Lakini home sijawahi kutuma hata mia/ Usiweke loud speaker wajomba wasije wakaniskia/ Halafu kaa nao kwa mbali ndo niweze kukuhadithia/ Nime sign huu mkataba, ili wanisimamie/ Shows, ma-collabo, madili wanitafutie/ Nikipiga picha na mapesa msichukie/ Kila nachofanya lazima wao ndo wanipangie/ Nimepangiwa Mbezi mama, huku ushuani/ Bahari inaonekana nikiwa kibarazani/ Mastaa na watu mashuhuri ndo majirani/ Na tunaalikana sana kwenye party za nyumbani/ Siulizwi kuhusu bili za umeme wala za maji/ Mabosi wangu katika lebo ndo mainchaji/ Iwe miswaki dawa za meno ama siagi/ Wanunuzi wao mi nakwenda kama mtumiaji/ Wifi muda wote niko tik tok live/ Nikitoka nacheza game tu PS five/ Nikizunguka uani kuna swimming na dive/ Na nikishaoga nacheki mamuvi full vibe/ Siku hizi napendeza navalishwa na maduka/ Kila baada siku mbili naletewa pamba mpya/ Sivai tena nguo za kupauka/ Mi popote ntakapoonekana nimewaka nimenyuka/ Yaani tukienda kila sehem mama/ Lazima nishobokewe na madem sana/ Kwa sababu nafanya poa kwenye game mama/ Na enjoy nafaidi matunda ya fame mama/ Nikihojiwa inabidi niseme nna pesa chungu nzima/ Mana itaua brandi ka nikionekana sina/ Kwa hiyo msije dhani labda nawanyima/ kwenye lebo hivi vitu kuvifanya ni lazima/ Mama kwenye kila milioni yangu laki/ Mana wao ndo wanannunulia jodani na mashati/ Majinzi nyomi yamejazana kwenye kabati/ Bado kila wiki napewa mialiko kwenye party/ Hahaha sasa hutaki mom/ Napiga mapicha mpaka na kina platinum/ Tunagonga Cheers tuna pop some/ Tunavaa ma- jewels flani made, but custom/ Tunapiga mastori na kina Zuchu/ Muda wote nipo katikati ya watu maarufu/ Mabaunsa wametuwekea ulinzi huku na huku/ Ili ufike mi nilipo mpaka wao wakuruhusu Tunaishi kijanja/ Night hatupoi piga misele kila kiwanja/ Kurudi getoni mida ya wanga/ Tushapiga tungi na misosi na kuruka sana kwanja/ Mabosi hawana noma kwenye bili/ Bata la bei ya chini kwa siku la laki mbili/ Machupa yakibaki nayastiri/ Yanaanzisha tena vibe tukipinduka siku ya pili/ Ila wasanii wenzangu wananicheka/ Mana mi napata sifa tu wao wanapata pesa/ Hata hili gari nlilopewa kuliendesha/ Ni mali ya lebo siondoki nalo siku ya kusepa/ Nasainishwa mikataba ya madili/ Lakini mipango ya pesa mabosi wanafanya siri/ Nikiuliza najibiwa kikatili/.... Dogo maisha yote unayoishi ni sisi ndo walipaji bili/ Na ni kweli nna raba chumba kizima/ Na pia kabatini nna pamba za kila aina/ Suti mbali mbali zinaagizwa toka china/ Natinga nawaka ila mfukoni hata kumi sina/ Kuna wakati natamani kuvunja mkataba/ Ila akaunti ndo kwanza ina laki tatu na buku saba/ Wakinitimua watachukua gari mpaka raba/ Mwisho wa siku mama ntapagawa nianze kula ngada/ Inaniuma sana unavyoishi kimaskini/ Wakati mwanao ndo msanii na hiti hapa mjini/ Lawama za ndugu zangu zote kwangu mimi/ Wanauliza "huo ustaa wake unatuongezea nini?" Show zenyewe nazopaform ni birthday/ Ama labda anazindua duka jipya vunja bei/ Mungu ananiongoza najilinda sipotei/ Mana tunalazimishwa kujimix na ma-gay/ Mmenilea vyema mmenifunza sana dini/ Tangu mdogo madrasa na ukubwani msikitini/ Lebo yangu imeshanifanya mtoto wa mjini/ Ni mwendo wa misuko chekibobu utanieleza nini/ Mama, mjomba shabani aliniomba kanzu/ Asione kimya mi bado nangoja mgao wangu/ Muhasibu anadai baada ya kupiga mahesabu/ Inaonekana mwaka mzima nimeingiza laki tatu/ Kusema kweli nimebugi ile kinoma/ Nimeingia kichwa kichwa pasipo mchezo kuusoma/ Na lebo kuniachia wanagoma/ Nilipe bilioni, na bado wanabakia na mangoma/